Pata taarifa kuu
IRAN-UKRAINE-CANADA-AJALI

Ajali ya ndege Tehran: Iran yakanusha madai ya Trudeau

Moja ya injini za ndege ya shirika la ndege la Ukraine International Air, Boeing 737-800 (yenye chapa PS752), iliyopatiana chini ya kifusi cha ndege hiyo, Tehran, Januari 8, 2020.
Moja ya injini za ndege ya shirika la ndege la Ukraine International Air, Boeing 737-800 (yenye chapa PS752), iliyopatiana chini ya kifusi cha ndege hiyo, Tehran, Januari 8, 2020. Iran Press/Handout via REUTERS

Taarifa za kiupelelezi zilizokusanywa na Canada zinaonyesha kwamba ndege ya Ukraine ambayo ilianguka karibu na mji wa Tehran Jumatano wiki hii inaweza kuwa ilidunguliwa kimakosa kwa kombora la Iran, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Justin Trudeau alitangaza Alhamisi wiki hii kwamba vyanzo kadhaa vya ujasusi, pamoja na vile vya Canada, vinaonyesha kwamba Boeing 737 ambayo ilianguka karibu na mji wa Tehran Jumatano wiki hii "ilidunguliwa na kombora la Iran".

"Tunayo taarifa kutoka vyanzo vingi, kususan taarifa kutoka kwa washirika wetu na idara zetu za usalama na upelelezi" ambazo "zinaonyesha kuwa ndege hiyo ilidunguliwa kwa kombora la Iran. Labda haikuwa kwa makusudi, "amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia amethibitisha Alhamisijioni kwamba Boeing 737 ilidunguliwa kwa kombora.

"Nina mashaka," amesema Donald Trump wakati alipoulizwa kuhusu sababu ya ajali hiyo. "Nina uhakika kuwa kitu kibaya kilitokea," ameongeza wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House.

Video ambayo imepewa gazeti la New York Times inaonyesha wakati ndege hiyo ilipodunguliwa kwa kombora mapema alfajiri muda mfupi baada ya kupaa hewani kutoka uwanja wa ndege ulio karibu na mji wa Tehran, amesema mwandishi wetu wa Washington, Anne Corpet. Mlio wa mlipuko unasikika lakini ndege iliendelea na safari yake, na kulazimika kurejea kwenye uwanja wa ndege ilikotoka, kabla ya kuanguka.

Kwa mujibu wa televieni za Marekani, maafisa kadhaa wa idara ya ujasuzi wanaamini kwamba Boeing 737ilidunguliwa kwa kombora la Iran.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.