Pata taarifa kuu
UFARANSA-CHINA-AFYA

Virusi vya Corona: Ufaransa yajiandaa kurudisha nyumbani raia wake kutoka Wuhan

Zoezi la kuwarudisha nyumbani litafanyika "katikati ya wiki," Waziri wa Afya Agnès Buzyn alisema baada ya mkutano huko Matignon, Januari 26, 2020.
Zoezi la kuwarudisha nyumbani litafanyika "katikati ya wiki," Waziri wa Afya Agnès Buzyn alisema baada ya mkutano huko Matignon, Januari 26, 2020. Lucas BARIOULET / AFP

Serikali ya Ufaransa kupitia Waziri wake wa Afya, Agnès Buzyn, imetangaza kwamba "itawarudisha nyumbani raia wake waishio katika mji wa Wuhan, kitovu cha mlipuko wa ugonjwa mpya unaofahamika kama 'Corona', nchini China, katikati ya wiki ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuwarudisha nyumbani raia wetu waishio Wuhan, nchini China, litafanyika "katikati ya wiki" kwa "makubaliano na viongozi waa China," Waziri wa Afya wa Ufaransa amesema. Zoezi hilo litafanyika chini ya usimamizi wa "timu maalumu ya matabibu ". Watakapowasili, watu hao "watabaki kwenye eneo la mapokezi kwa muda wa siku 14", kipindi kinacholingana na kipindi cha kuonekana dalili za mtu aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa mpya unaofahamika kama 'Corona'.

Agnes Buzyn amekadiria kuwa idadi ya watu wanaohusika kwa zoezi hilo inaweza "kuanzia zaidi ya kumi hadi zaidi ya mia moja". Maafisa kwenye balozi zetu nchini China "wameanza kuorodhesha" wale wanaotaka kurudi, wengine wanaweza kusita kwa sababu ya kipindi cha karantini ambacho kimewekwa kuzuia "kusambaa kwa virusi katika ardhi ya China", Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnès Buzyn amesema.

Vifo vinavyosababishwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo vimeongezeka nchini China na kufika watu 41, katika siku ya mwaka mpya wao.

Vifo vingine 15 vilitokea katika jimbo la Hubei, eneo ambalo virusi hivyo vilianzia, ilitangazwa siku ya jumamosi.

Maafisa wa afya bado wanajaribu kutafuta tiba au kinga ya virusi hivyo kwa kuwa mlipuko wa ugonjwa huo umetokea kipindi ambacho mamilioni ya raia wa China wanasafiri kwa ajili ya sherehe muhimu nchini humo ya mwaka mpya. Matamasha mengi yamezuiliwa kufanyika katika kipindi hiki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.