Pata taarifa kuu
URUSI-CHINA-AFYA

Coronavirus: Urusi yafunga mipaka yake ya ardhini na China

Le président Vladimir Poutine tient une réunion de crise sur le coronavirus, le 29 janvier 2020, à Moscou.
Le président Vladimir Poutine tient une réunion de crise sur le coronavirus, le 29 janvier 2020, à Moscou. Alexei Druzhinin / SPUTNIK / AFP

Urusi inataka kupambana dhidi ya Ugonjwa hatari unaofahamika kama Corona, ambao umekuwa ni tishio duniani. Serikali ya Urusi imeamua kufunga mipaka yake ya ardhini na China ili kuzuia maambukizi yoyote kutoka China kuingia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umewekwa wazi Alhamisi hii, Januari 30 na Waziri Mkuu mpya wa Urusi, Mikhaïl Michoustine. Urusi bado haijaorodhesha kesi yoyote ya maambukizi kwenye aridhi yake, lakini wafanyikazi wengi wa China na watalii wako au waliwahi kuwa nchini Urusi.

Urusi ina zaidi ya kilomita 4,000 za mpaka na China, na jumla ya mikoa mitano itakuwa chini ya uamuzi huo, huko Siberia na Mashariki ya Mbali ya Urusi. Hatua hiyo inaanza kutumika leo Alhamisi; ni ya muda imebainisha serikali, bila hata hivo kutoa tarehe muda wa mwisho. Hatua nyingine iliyochukuliwa na Urusi ni kwamba raia wa China hawataweza tena kupata visa vya elektroniki ambavyo viliwawezesha kusafiri kwa majimbo ya Mashariki ya Mbali, Saint Petersburg na eneo la Kaliningrad.

Urusi itapungukiwa na dola milioni 100 kutokana na hatua hiyo.

Kwa wastani, watalii wa China milioni 1.5 hutembelea Urusi kila mwaka. Upungufu huo unaweza kuwa mkubwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.