Pata taarifa kuu
CHINA-WHO-AFYA

WHO yatangaza ugonjwa wa Corona kuwa janga la dunia

Maafisa wa afya wakikagua wasafiri kama sehemu ya utaratibu wa kufanya vipimo vya ugonjwa wa Corona kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kotoka huko Accra, Ghana, Januari 30, 2020.
Maafisa wa afya wakikagua wasafiri kama sehemu ya utaratibu wa kufanya vipimo vya ugonjwa wa Corona kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kotoka huko Accra, Ghana, Januari 30, 2020. REUTERS/Francis Kokoroko

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ugonjwa hatari unaofahamika kama Corona ulioanzia katika mji wa Wuhan, nchini China, kuwa janga la dunia.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linapinga hatua ya kusitisha safari na biashara na nchi ya China.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametangaza uamuzi huo baada ya kikao cha dharura cha kamati ya mseto ya shirika hilo.

"Sababu kubwa ya tangazo hilo si kwa sababu ya kile ambacho kinatokea China kwa sasa lakini kile ambacho kinatokea katika mataifa mengine," alisema kiongozi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus .

Akizungumza katika mkutano wa habari Geneva, Dkt Tedros alielezea virusi vya corona kuwa mlipuko wa ugonjwa ambao haujawahi kutokea awali na bado haujaweza kupata suluhu.

Dkt.Tedros alisifia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya China katika kuzuia maambukizi yasienee na alisema kuwa hakukuwa na sababu ya kuzuia watu wasisafiri au biashara zisiendelee.

Ugonjwa wa Corona umeua watu 170 na watu 8,100 wameambukizwa ugonjwa huo, huku ukiendelea kuwa kitisho kwa mataifa mengi duniani hasa nchi jirani na China.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.