Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-AFYA

Mgonjwa mpya aliyeambukizwa virusi vya Corona afariki Hong Kong

Picha hii iliyopigwa Januari 28, 2020 inaonyesha maafisa wa afya wakimpa matumaini ya kupona mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa unaofahamika kama Corona katika hospitali ya Zouping katika jimbo la Shandong.
Picha hii iliyopigwa Januari 28, 2020 inaonyesha maafisa wa afya wakimpa matumaini ya kupona mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa unaofahamika kama Corona katika hospitali ya Zouping katika jimbo la Shandong. STR / AFP

Serikali ya China imekubali kukabiliana na changamoto mbalimbali katika vita dhidi ya virusi vya ugonjwa unaofahamika kama Corona, ambao umezua hofu ulimwenguni.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Kufikia siku ya Jumatatu, watu 425 wamefariki dunia nchini China na wengine 20,000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, huku ripoti zikisema kuwa 3,000 huambukizwa kila siku.

Katika hatua nyingine eneo la Hong Kong, limeripoti kifo chake cha kwanza, huku kiongozi wa eneo hilo Carrie Lam amesema, uongozi wake unafanya kila kinachowezekana kukabiliana na hali hiyo.

Msemaji wa hospitali amesema kuwa mtu huyo aliyefariki dunia alikuwa na umri wa miaka 39 na alikuwa mkazi wa Hong Kong, ambaye Januari 21 alisafiri kwenda mji wa China wa Wuhan, eneo ambalo ugonjwa unaofahamika kama Corona ulianzia, kabla ya kurudi Hong Kong siku mbili baadaye.

Wakati huo huo mamlaka nchini Japan Jumanne wiki hii inachunguza afya ya watu 3,711 waliowekwa karantini katika meli moja karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Tokyo, baada ya kesi moja ya maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa abiria kuthibitishwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.