Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA-HAKI

Zaidi ya watu 700 wakamatwa na wengine watafutwa Uturuki

Vikosi maalum vya Uturuki mbele ya Mahakama ya Ankara, ambapo baadhi ya maafisa wa polisi walilengwa kwa risasi Jumatatu Julai 18.
Vikosi maalum vya Uturuki mbele ya Mahakama ya Ankara, ambapo baadhi ya maafisa wa polisi walilengwa kwa risasi Jumatatu Julai 18. ADEM ALTAN / AFP

Zaidi ya watu 700, wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini Fethullah Gülen, wanaoshukiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwaka 2016, wamekamatwa au wanakabiliwa na waranti wa kukamatwa nchini Uturuki, shirika la habari la serikali Anadolu limetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Katika uchunguzi uliofanywa katika jeshi la Uturuki, waendesha mashitaka nchini Uturuki wameagiza kukamatwa watu 157 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na mhubiri wa kidini aliye uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka1999 na ambaye anakanusha kuhusika kwake katika jaribio hilo la mapinduzi.

Kwenye Wizara ya Sheria watu 71 pia wanatakiwa kukamatwa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu uungwaji wao mkono kwa Fethullah Gülen, limesema shirika la habari la Anadolu.

Wakati huo huo, waendesha mashtaka wametoa vibali vya kukamatwa kwa watu 467 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na Gülen kama sehemu ya uchunguzi wa kesi za ufisadi katika polisi.

Tangu kuanza kwa operesheni kubwa ya kamata kamata kuhusu jaribio la mapinduzi, watu wapatao 80,000 wamewekwa kizuizini na wafanyakazi wengine wa serikali 150,000 wamekamatwa au kusimamishwa kazi, hasa katika sekta ya elimu na katika jeshi.

Wapinzani wa rais Recep Tayyip Erdogan wanamtuhumu rais huyo kwa kutumia jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwaka 2016 kama kisingizio cha kukandamiza mtu yeyote anathubutu kufungua mdomo kwa kukosoa utawala wake.

Serikali imekanusha madai hayo na kubaini maswala ya usalama wa kitaifa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.