Pata taarifa kuu
CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: China yatangaza visa vipya 62 vya maambukizi

Idadi ya waathiriwa wa ugonjwa wa Covid-19 yaendelea kutia mashaka nchini China.
Idadi ya waathiriwa wa ugonjwa wa Covid-19 yaendelea kutia mashaka nchini China. Hector RETAMAL / AFP

Mamlaka ya afya nchini China imethibitisha visa vipya 62 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambapo janga hilo lilizuka mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Siku moja kabla watu 32 waliambukizwa virusi vya Corona, kwamujibu wa mamlaka ya afya.

Vifo viwili vya nyongeza vinavyohusiana na COVID-19 vimeripotiwa, Tume ya kitaifa ya afya imesema katika mkutano wake la kila siku na waandishi wa habari.

Kulingana na ripoti ya tume hiyo, visa 81,802 vya maambukizi na vifo 3,333 vimeripotiwa nchini China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo.

Wakati huo huo mamlaka nchini China imeondoa marufuku ya kukaa nyumbani katika mji wa Wuhan, ambako ugonjwa wa Covid-19 ulianzia, baada ya miezi miwili wakaazi wa mji huo kutotoka nje.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.