Pata taarifa kuu
CHINA-WHO-CORONA-AFYA

China kutoa Dola Milioni 30 kwa WHO

Virusi vya Corona vimeua watu wengi China, hasa katika mji wa Wuhan, kitovu cha ugonjwa huo.
Virusi vya Corona vimeua watu wengi China, hasa katika mji wa Wuhan, kitovu cha ugonjwa huo. Hector RETAMAL / AFP

China inasema itatoa mchango wa Dola Milioni 30 kwa Shirika la Afya Duniani WHO, kulisaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, ugonjwa unaosubua ulimwengu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje nchini humo Hua Chunying kupitia ukurasa wake wa Twitter amethibtisha hilo na kusema mchango huo unalenga kulisaidia shirika hilo kupambana virusi katika nchi zinazoendelea.

Aidha, amesema kuwa tayari China imetoa Dola Milioni 20, mchango uliotoa kwa WHO mwezi Machi.

Hatua hii ya China imekuja wiki moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa nchi yake inasitisha mchnago Wake kwa Shirika hilo kwa madai ya kushindwa kudhibiti mapema kwa virusi hivyo.

Hatua hiyo ya Marekani ambayo inasalia mchangiaji mkunbwa kwa Shirika hilo, lilaaniwa na China na mataifa mengine ya Magharibi huku WHO ikisema huu sio wakatoi wa kusitisha mchnago huo wa fedha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.