Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-CONGO-AFCON-SOKA-MICHEZO

Congo na Equatorial Guinea zatoka sare

Beki wa Equatorial Guinea Sipo Bohale na mshambuliaji wa Congo Dominique Malonga (kushoto) katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la mataiafa ya Afrika Januari 17mwaka 2015 katika uwanja wa Bata.
Beki wa Equatorial Guinea Sipo Bohale na mshambuliaji wa Congo Dominique Malonga (kushoto) katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la mataiafa ya Afrika Januari 17mwaka 2015 katika uwanja wa Bata. AFP

Timu ya taifa ya Congo imetoka sare ya bao moja kwa moja na Equatorial guinea katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika kundi A, inayochezwa nchini Equatorial Guinea.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyeji wa michuano hiyo, Equatorial Guinea, imeongoza katika kipindi cha kwanza kwa bao 1 kwa 0 dhidi ya Congo. Bao ambalo limeingizwa katika dakika ya 16 ya mchezo.

Bao hilo la Equatorial Guinea limepachikwa wavuni na Nsue Lopez, baada ya kupewa pasi na Edu Salvador.

Hata hivyo katika kipindi cha pili, Congo imekuja juu, hadi katika dakika za nyongeza timu hiyo ikasawazisha. Bao ambalo limewekwa kimyani na mchezaji machachari Bifouma, ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Espoirs ya Ufaransa, na kuwatuliza tumbo joto wachezaji na mashabiki wa timu ya taifa ya Congo ambao walikua walishakata tamaa.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea, Nsue Lopez na Edu Salvador, wameoneka kutamba uwanjani, huku mabeki wa Congo wakihangaika na kujiuliza vipi watadhibiti wachezaji hao. Katika dakika ya 70, timu ya taifa ya Congo imeponea kuingizwa bao la pili, baada ya nahodha wa Equatorial Guinea kuelekeza mkwaju kwenye lango la Congo.

Hata hivyo Balboa, mshambuliaji makini, ambaye aliwahi kuingiza bao wakati wa mechi ya kwanza ya Nzalang katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika (mwaka 2012 katika uwanja wa Bata), ameonekana akitamba uwanjani. Lakini alikosea bao baada ya kukosana na golkipa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.