Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-CONGO-AFCON-SOKA-MICHEZO

Gabon - Burkina Faso zamenyana lakini hakuna uadui

Mchezaji wa Gabon, Bruno Ecuele Manga (kulia)akikabiliana na mchezaji wa Burkina Faso, Koffi Ouedraogo wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2012.
Mchezaji wa Gabon, Bruno Ecuele Manga (kulia)akikabiliana na mchezaji wa Burkina Faso, Koffi Ouedraogo wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2012. AFP PHOTO/YANICK MANIENGUI

Mchuano kati ya timu ya za taifa za soka za Gabon na Burkina Faso, Januari 17 katika uwanja wa Bata nchi Equatorial Guinea, ni mechi ya pili itakayochezwa leo katika kundi A baada ya mechi kati aEquatoria Guinea na Congo. 

Matangazo ya kibiashara

Timu hizo mbili ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kuongoza katika kundi A zilichuana mara kadha katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, hakuna uadui kati ya timu hizo, wamesema makocha wa timu hizi mbili.

Timu za Gabon na Burkina Faso zinachuana leo Jumamosi Januari 17 kwa mara ya saba tangu mwaka 2010 katika uwanja wa Bata, katika duru ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.

Mataifa hayo mawili yalikutana katika michuano ya kufuzu ya Kombe la dunia 2014 na katika michuano ya Kombe la mataifa ya AfrikaCAN 2015.

Paul Put, kocha wa Burkina Faso, anakubaliana na hoja hiyo: " tunasema kwamba tutachuana na Gabon ambayo inachezea nyumbani. Wengi wa mashabiki wake watakuja kuhudhuria mechi kwa sababu michuano hiyo inachezwa karibu ya nchi yao. Kwa upande wetu, mchezo huu ni kama safari. Tunajua thamani ya Gabon. Hii ni timu nzuri sana. Mchezo huu utakua mgumu", amesema Paul Put.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.