Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Algeria yairejesha nyumbani Senegal

Mchezaji wa Senegal Papa Diop Kouly akimkabili na kuvuta jezi la mchezaji wa Algeria Yacine Brahimi.
Mchezaji wa Senegal Papa Diop Kouly akimkabili na kuvuta jezi la mchezaji wa Algeria Yacine Brahimi. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Timu ya taifa ya Algeria imeifunga Senegal mabao 2-0, Jumanne wiki hii jioni katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika inayo endelea.

Matangazo ya kibiashara

Algeria imefuzu katika robo fainali ya michuano hiyo huku Senegal ikishindwa na hivyo kurejea nyumbani, baada ya kuchukua nafasi ya tatu nyuma ya ya Ghana ambyo imeiburuza Afrika Kusini mabao 2-1.

Ni kwa mara ya tatu, baada ya mwaka 2008 na mwaka 2012, Senegal inaondolewa katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika hatua ya kwanza. Senegal imelazimika kurejea nyumbani baada ya kuburuzwa kwa mabao 2-0 Jumanne Januari 27, wakati wa michuano iliyozikutanisha timu za kundi C.

Bao la kwanza la Algeria lilifungwa na Riyad Mahrez, kiungo wa kati, katika dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

Katika dakika ya 28, Senegal imemkosa mchezaji wake nyota, kiungo wa kushoto, Cheikh Mbengue, ambae aliondolewa uwanjani kutokana na jeraha alilopata kichwani alipokua akikabiliana na kiungo wa kulia wa Algeria, Aïssa Mandi.

Kabla ya kwenda mapumzikoni, Algeria ilikua ikiongoza kwa bao 1-0. Katika dakika ya 81, Nabil Bentaleb, alifaulu kuweka kimyani bao la pili la Algeria. Hadi kipenga cha mwisho Senegal ilijikuta ikiienda patupu, na kuaga mashindano.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.