Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Mashetani Wekundu waburuzwa kwa mabao 4-2

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mazoezi, Januari 18 mwaka 2013.
Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mazoezi, Januari 18 mwaka 2013. RFI / David Kalfa

Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika imeingia katika hatua ya robo fainali Jumamosi Januari 31. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeiburuza Congo Brazaville kwa mabao 4-2.

Matangazo ya kibiashara

Hadi muda wa mapumziko timu hizi mbili zilikua hazijafungana bao hata moja. Katika kipindi cha pili Congo Brazaville imekuja juu na kuanza kuingiza bao la kwanza katika dakika ya 53 ya mchezo.

Congo Brazaville imeendelea kulisakama lango la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kufaanikiwa kuingiza bao la pili katika dakika ya 60 ya mchezo.

Licha ya kuwa safa ya ulinzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekua imeshindwa kudhibiti washambuliaji wa Mashetani Wekundu wa Congo Brazaville, ilifaulu kuingiza bao la kwanza, baadae matokeo yakabadilika.

Bao hlo la kwanza la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeingizwa katika dakika ya 65 ya mchezo.

Hata hivyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haikukomea hapo, ilikuja juu na kulishambulia lango la Mashetani Wekundu na kufanikisha kuingiza bao la kusawazisha, na kubadili matokeo kuwa 2-2.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeendelea kulishambulia lango la Mashetani Wekundu, baada ya kuvuja kwa safu ya ulinzi ya Congo Brazaville. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliingiza bao la tatu, na baadae bao la nne.

Hadi dakika 90 za mchezo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya imekua ikiongoza kwa mabao 4-2.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.