Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

DRC na Cote d'Ivoire katika mchuano wa nusu fainali

Mchezaji wa DRC, Jeremy Bokila (kushoto), mchezaji wa Cote d'Ivoire(kulia).
Mchezaji wa DRC, Jeremy Bokila (kushoto), mchezaji wa Cote d'Ivoire(kulia). REUTERS/Hutchings & Abdallah Dalsh - AFP / DE SOUZA –Montage RFI

Timu za taifa za soka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Cote d'Ivoire zitajitupa uwanjani Alhamisi wiki hii kwa mchuano wa nusu fainali, kuwania taji la ubingwa wa Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa Jumatano Februari 4 katika uwanja wa Bata nchini Equatorial Guinea kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Maashariki sawa na saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati.

Mataifa haya mawili yalimenyana mwaka uliopita katika mechi ya kufuzu kucheza fainali hizi, DRC walifungwa mabao 2 kwa 1 nyumbani na walipokwenda Abidjan waliwafunga Cote d'Ivoire mabao 4 kwa 3.

Hii ni wazi kuwa mechi haitakuwa rahisi Jumatano wiki hii, na kocha wa Leopard Florent Ibenge atakuwa anataka kudhirihisha kuwa ana uwezo wa kuiongoza timu yake kufika fainali, sawa na Mfaransa Herve Renard ambaye lengo lake ni kuhakikisha kuwa Cote d'Ivoire inanyakua taji hilo walilonyakua mwisho mwaka 1992.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.