Pata taarifa kuu
MALAWI

Wanawake nchini Malawi kuandamana kesho.

Wanawake nchini Malawi wakiwa katika mavazi tofauti na suruali
Wanawake nchini Malawi wakiwa katika mavazi tofauti na suruali globalpost.com

Wanawake katika miji mbalimbali nchini Malawi wanatarajiwa kufanya maandamano kesho Ijumaa, kudai haki yao kuvaa suruali. 

Matangazo ya kibiashara

Seodi White mwanaharakati wa maswala ya haki za biandamu na wanawake nchini humo, amesema maandamano hayo yatafanyika baada ya polisi hapo jana kulikamata genge la watu ambalo limekuwa likiwavua wanawake suruali ndefu mjini Lilongwe.

Polisi wanasema visa hivyo vimekuwa vikifanywa na vijana ambao hawana ajira, na wamekuwa wakiwaandama wanawake hao.

Kuvuliwa suruali ndefu kwa wanawake nchini humo kunaleta kumbukumbu ya miaka ya mwanzoni mwa tisini ambayo serikali ya kidteta Kamuzu Banda ilipiga marufuku wanawake kuvaa nguo za ndani, marufuku iliyoondolewa mwaka 1994.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.