Pata taarifa kuu
MAREKANI

Jim Yong Kim ateuliwa kuwa mkuu mpya wa benki ya Dunia

Jim Yong Kim mkuu mpya wa benki ya dunia
Jim Yong Kim mkuu mpya wa benki ya dunia Reuters

Benki ya Dunia imemchagua Jim Yong Kim raia wa Marekani mwenye asili ya Korea kushika wadhifa wa kuongoza Taasisi hiyo kubwa duniani kifedha uteuzi ambao unatajwa kuwashangaza wengi kwani alikuwa hapewi nafasi kubwa. 

Matangazo ya kibiashara

Kim ambaye kitaaluma ni mtu aliyebobea kwenye masuala ya Afya na Elimu amemuangusha Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala ambaye amekubaliana na uamuzi huo huku akisema hiyo haijamkatisha tamaa.

Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza uteuzi huo akisema ulifanyika kwa uhuru na haki na sasa Kim anatarajiwa kuchukua nafasi ya Robert Zoellick ambaye anamaliza muda wake mnamo mwezi June mwaka huu.

Wachambuzi wa mambo wamekosoa uteuzi wa kiongozi huyo wakisema kuwa uteuzi wake haukuzingatia taaluma ta masuala ya uchumi ambayo ndio ingekuwa kigezo kikubwa kwa mkuu wa benki ya dunia kuwa.

Wachambuzi hao wameongeza kuwa, uteuzi huo umeendelea kudhihirisha ukoloni mambo leo wa taifa la Marekani ambalo mara zote limekuwa likifanikiwa kumteua mtu ambaye amekuwa akishinda nafasi hiyo na kuendelea kuhodhi kiti hicho.

Mwezi March mwaka huu rais Barack Obama alimtangaza Kim kama chaguo la nchi yake kushika wadhifa huo huku akisema kuwa amefanya makubwa kwa dunia wakati akiwa mkuu wa shirika la Afya WHO pamoja na mshauri wa masuala ya HIV/AIDS.

Waziri wa fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo amepongeza uteuzi wa kiongozi huyo akisema kuwa ameridhika na uteuzi wake akiamini kuwa malengo ya benki hiyo yatafikiwa japo alikuwa akipewa nafasi kubwa kwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.