Pata taarifa kuu
Pakistani

Serikali ya Pakistani yaifukuza familia ya Bin Laden

Nyumba ambayo Ben Laden muasisi wa mtandao wa alqaeda alimokuwa anaeshi kabla ya kifo chake mei 2 mwaka 2011, ambayo imeanza kubomolewa na serikali ya Pakistani tangu mwezi februari 2012.
Nyumba ambayo Ben Laden muasisi wa mtandao wa alqaeda alimokuwa anaeshi kabla ya kifo chake mei 2 mwaka 2011, ambayo imeanza kubomolewa na serikali ya Pakistani tangu mwezi februari 2012. AFP PHOTO/ AAMIR QURESHI

Serikali ya Pakistani imeifurusha familia ya Bin Laden Ijumaa hii April 27, 2012. Wajane watatu na watoto zaidi ya kumi wa hayati Ben laden muasisi wa mtandao wa Alqaeda, ambao walikuwa wanaziuliwa na serikali ya Islamabad tangu kutokea kifo cha Osama Ben Laden. wajane wa Osama Ben Laden na watoto kumi na moja wameondoka nchini Pakistani mapema Ijumaa hii kwa ndege maalum kuelekea nchini Saudi Arabia. wawili kati ya wajane hao ni raia wa Saudia Arabia, huku mwengine akiwa ni raia kutoka Yemen. 

Matangazo ya kibiashara

Mjane mmoja ambae ni raia wa Yemen atapelekwa nchini mwake na wanae watano. kufurushwa kwa familai ya Ben Laden nchini Pakistani, serikali ya Islamabad inataka kufunga ukurasa wa historia ya Alqaeda nchini Pakistani, historia ambayo nchi hiyo haikupenda kuweka bayana.

Osama Ben Laden aliuawa na jeshi la Marekani Mei 2 mwaka 2011 katika ardhi ya Pakistani katika mji uliokwenye umbali wa saa mbili kuelekea mji mkuu Islamabad, hali ambayo ilipokelewa na serikali ya Pakistani kwamba ni dharau kubwa dhidhi yake na ilionekana kuchafuwa picha ya nchi hiyo kimataifa.

Wajane hao wameachwa huru Ijumaa hii, takriban mwaka mmoja baada ya kifo cha muasisi wa Alqaeda, lakini kabla ya hapo walikuwa chini ya ulinzi bila sababu yoyote, kabla ya kufungwa siku 45 baada ya kukutwa na hatia ya kueshi nchini Pakistani bila kibali maalum.

Katika kipindi hicho cha siku 45, mengi yalitolewa kuhusu maisha ya Osama Ben Laden. Mke mdogo wa hayati huyo alifahamisha kuwa uduwi namba moja wa Marekani aliishi katika mji minne tofauti nchini Pakistani, na wakati alipopewa ujauzito mara mbili kujifungua katika hospitali za taifa huku akitumia majina bandia

Hata hivyo mwaka mmoja baada ya kifo cha Osama Ben Laden, masuali mengi bado yanaibuka kuhusu kukimbia kwake na kueshi nchini Pakistani kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi bila kuwa na wasiwasi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.