Pata taarifa kuu
Syria-Urusi

Vikwazo vya Marekani kwa Syria Urusi yaumia kibiashara,yataka kujadili mpango wa amani wa Geneva na baraza la usalama la UN

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov,
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, REUTERS/Denis Sinyakov

Vikwazo vya marekani dhidi ya Syria na Iran vinatishia maslahi ya kibiashara kwa nchi ya Urusi ,waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amebainisha.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ameyasema hayo baada ya mkutano wake na waziri wa mambo ya kigeni wa marekani Hilary Clinton na kuongeza kuwa vikwazo kwa mataifa hayo vinatishia hali ya nchi yake kibiashara.

Aidha waziri Lavrov amesema pia upo mpango wa kufanya mkutano maalum na baraza la usalama la umoja wa mataifa UN utakaoshirikisha mawaziri kujadili mpango wa amani nchini Syria.

Urusi imetuhumiwa na jumuiya za kimataifa kuunga mkono utawala wa raisi Assad ambao umekuwa ukimwaga damu ya raia wasio kuwa na hatia na kusababisha raia kukimbia makazi yao.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.