Pata taarifa kuu
VENEZUELA-CUBA

Wananchi wa Venezuela washerehekea Mwaka Mpya kwa kumuombea Rais Chavez apate ahueni

Wafuasi wa Rais Hugo Chavez wakiwa kwenye maombi maalum kwa ajili ya kumuombea Kiongozi wao apate ahueni
Wafuasi wa Rais Hugo Chavez wakiwa kwenye maombi maalum kwa ajili ya kumuombea Kiongozi wao apate ahueni REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Hugo Chavez wameukaribisha mwaka mpya wa 2013 kwa kufanya maombi kutokana na hali ya afya ya Kiongozi wao kuwa mbaya huku wakisitisha sherehe na shamra shamra zote zilizokuwa zimeandaliwa.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya Wafuasi wa Rais Chavez wamejitokeza kwenye sehemu za ibada na maeneo ya wazi na kufanya maombi maalum wakimuomba kheri kiongozi wao ambaye anaendelea kupatiwa matibabu nchini Cuba.

Maombi haya yanakuja siku moja baada ya Makamu wa Rais na Mrithi wa Kisiasa wa Rais Chavez, Nicolas Maduro ndiye alitoa taarifa ambazo zilionekana mbaya kwa wananchi baada ya kueleza hali ya afya ya Kiongozi huyo imezidi kuwa mbaya.

Tamko hilo la Makamu wa Rais Maduro ndilo liliwafanya wananchi na wafuasi wa Rais Chavez kuchukua uamuzi wa kuendesha maombi maalum huku wakiahirisha sherehe zote ambazo zimeandaliwa.

Maombi hayo ya wananchi wa Venezuela yanakuja baada ya Makamu wa Rais Maduro kutangaza Rais Chavez anakabiliwa na tatizo jingine ukiondoa lile la upumuaji lililobainika pindi baada ya kufanyiwa upasuaji wa saratani.

Tangu Rais Chavez agundulike kuwa na maradhi ya saratani ameshafanyiwa upasuaji mara nne nchini Cuba kwa lengo la kukabiliana na saratani hiyo lakini hali yake imeanza kudorora tofauti na wengi walivyokuwa wanadhani.

Licha ya Rais Chavez kuendelea kupatiwa matibabu taarifa za ndani ya nchi hiyo zinasema mpango wa kumuapisha upo pale pale kwani zoezi hilo litafanyika tarehe kumi ya mwezi januari mwaka 2013.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.