Pata taarifa kuu
IRAN

Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Amano akiri hakuna hatua zilizopigwa kwenye mazungumzo ya nyuklia na Serikali ya Iran

Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Yukiya Amano akihutubia kutoka Makao Makuu ya Shirika hilo huko Vienna
Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Yukiya Amano akihutubia kutoka Makao Makuu ya Shirika hilo huko Vienna Reuters

Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA limekiri hakuna hatua zozote zilizopigwa baina yake na Iran katika suala ka nyuklia inayozalishwa na Tehran taarifa inayokuja baada ya kufanyika mikutano kumi tofauti ambayo yote imevunjika bila ya kupatikana suluhu yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Shirika la IAEA Yukiya Amano ameiambia Bodi ya Magavana katika mkutano na kusema hadi kufika sasa hakuna hatua yoyote chanya ambayo imepigwa kwenye kupata uvumbuzi wa sauala hilo la nyuklia kwa Iran.

Amano amesema kwa namna ambavyo mchakato huo unaendeshwa ni wazi kabisa hakuna muelekeo mwema wa kumalizwa kwa suala hilo la nyuklia ambalo limekuwa likichangia Tehran kuwekewa vikwazo.

Mkuu wa Shirika la IAEA ameweka bayana kwa mwenendo uliopo itakuwa ngumu sana kupatiwa suluhu kwa tatizo hilo ambapo wao wanataka kujiridhisha iwapo kwenye matumizi yake hayana madhara kwa wengine.

Amano amesema lengo wao ni kutaka kumalizwa kwa suala hili lenye utata ili waweze kutekeleza wajibu wao na kutaka serikali ya Tehran kuwaruhusu waangalizi wao kwenda kujiridhisha kama kweli hawatengenezi silaha za nyuklia.

Tamko la Mkuu wa Shirika la IAEA limezidisha hofu ya kufikiwa makubaliano juu ya suala la kuzalishwa kwa nyuklia kunakofanywa na serikali ya Tehran ambayo yenyewe inasema inatumia kuzalisha nishati ya umeme.

Serikali ya Iran imekuwa ikishiriki kwenye mazungumzo ya pande sita lakini mara zote imekuwa ikikataa kuwaruhusu waangalizi kutoka IAEA kwenda Tehran kuchunguza shughuli ambazo wanazifanya kwenye uzalishaji huo wa nyuklia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.