Pata taarifa kuu
Sri Lanka

Mkutano wa Jumuiya ya Madola kutamatika leo Jumapili mjini Colombo

Viongozi wa Jumuiya ya Madola katika mkutano  mjini  Colombo nchini Sri Lanka
Viongozi wa Jumuiya ya Madola katika mkutano mjini Colombo nchini Sri Lanka Reuters/Sri Lankan President's Office/Handout

Viongozi wa Jumuiya ya Madola leo Jumapili wanatamatisha mkutano wao wa kilele huko Colombo nchini Sri Lanka, wakitarajiwa kuweka msimamo wa pamoja baada ya mazungumzo yaliyotawaliwa na mgogoro mkali kuhusu madai ya uhalifu wa kivita. 

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wanatarajiwa kutoa kauli ya pamoja katika masuala kama vile usimamizi wa fedha za madeni naufadhili ili kupambana na tishio la mabadiliko ya hali ya hewa kwa nchi ndogo kabla ya kutoka nje ya Colombo.

Hata hivyo mwonekano wa umoja hautasaidia zaidi ya kuficha mgawanyiko ndani ya safu ya Jumuiya ya Madola baada ya siku tatu ya mazungumzo ambayo yametawaliwa na tuhuma za kumalizika kwa vita ya miaka 37 nchini Sri Lanka mwaka 2009 iliyosababisha umwagaji damu mkubwa.

Mkutano huo ulianza kushughulikia mikakati kadhaa ya bodi hiyo kabla ya kuanza na viongozi wa Canada, India na Mauritius wote wakiamua kuamua kujitenga na mkutano huo kupinga rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Colombo.

Aidha Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alipata umaarufu zaidi ya mkutano huo katika siku ya ufunguzi kwa kufanya ziara ya kihistoria kwenye jimbo lililoathiriwa na vita la Jaffna ambapo alikutana na waathirika wa mgogoro ambao uliua watu zaidi ya 100,000.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.