Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP

Trump aweka wazi sera zake za nje

Washington, Aprili 27, 2016. Donald Trump alizungumzia kuhusu maono yake ya nafasi ya Marekani duniani.
Washington, Aprili 27, 2016. Donald Trump alizungumzia kuhusu maono yake ya nafasi ya Marekani duniani. REUTERS/Jim Bourg

"Marekani kwanza" ni kauli iliyorejelewa mara kwa mara na Donald Trump Jumatano hii mjini Washington.Trump ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda kura za mchujo katika chama cha Republican amesema anataka kuona sera za nje za Marekani katika mwelekeo pekee wa nchi yake.

Matangazo ya kibiashara

Si mara ya kwanza Donald Trumpa anatamka maneneo hayo. Inaonekana wazi kwamba Trump haziungi mkono sera za nje za marekani katika utawala wa Barack Obama, ambapo amekosoa jinsi Marekani inajihusisha wakati huu hasa na vita mbalimbali dhidi ya ugaidi, mpango wa nyuklia wa Iran, mahusiano ya nchi hiyo na Israel pamoja na China.

"Sera zangu za nje iitatetea maslahi ya Wamarekani na usalama wa Marekani kabla ya yote" amesema Trump Jumatano, Aprili 27 mjini Washington, akilenga washirika wakuu ambao hawashiriki vya kutosha katika huhudi za vita za Kimarekani, amesema bilionea huyo

Donald Trump amezitaja nchi kama Japan na Korea Kusini ambazo bado zina makambi mengi ya jeshi la Marekni katika ardhi zao.

"Tumegharimu maelfu ya mabilioni ya dola kwa kununua ndege, makombora, meli, vifaa, tumewekeza katika jeshi letu ili kutetea maslahi ya mabara ya Ulaya na Asia. nchi ambazo tunatolea ulinzi zinapaswa kulipia gharama ya ulinzi huo," amesisitiza mgombea wa chama cha Republican katika kura za mchujo, "au ikiwezekana wajilindie wao wenyewe nchi zao", Bw Trump ameongeza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.