Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Trump: Nafikiri Korea Kaskazini sasa inataka amani

Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia)  na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (Kushoto)
Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (Kushoto) AFP

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anafikiri kuwa Korea Kaskazini sasa inataka amani ya kudumu baada ya wito wake wa kuja katika meza ya mazungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Trump imekuja wiki hii baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuomba kuja katika meza ya mazungumzo na Marekani ili kumaliza tofauti zao ambazo zimetishia usalama wa dunia kwa muda mrefu.

Rais Trump amewaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Pennsylvania, kuwa wakati umefika kwa amani hiyo kurejea huku akisisitiza kuwa Marekani imeonesha uwezo wake dhidi ya Korea Kaskazini.

Kuelekea katika mazungumzo hayo ambayo yameratibiwa kufanyika mwezi Mei, Korea Kaskazini imekubali kusitisha majaribio ya silaha zake za maangamizi kama ambavyo imekuwa ikishuhudiwa katika siku zilizopita.

Mara ya mwisho kwa Korea Kaskazini kujaribu makombora yake ilikuwa ni tarehe 28 mwezi Novemba mwaka 2017.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.