Pata taarifa kuu
EAC-EU

Wabunge wa Ulaya, wakosoa mkataba wa EPA, wapongeza viongozi wa EAC kutotia saini

Baadhi ya wabunge wa bunge la Ulaya wakiwa kwenyhe moja ya vikao vyao
Baadhi ya wabunge wa bunge la Ulaya wakiwa kwenyhe moja ya vikao vyao europarl.europa.eu/portal

Baadhi ya wabunge wa bunge la umoja wa Ulaya wamesema kuwa, nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hazipaswi kukurupuka na kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo na umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya wabunge hao, wanaitoa wakati huu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wamejipa muda wa miezi mitatu, kuendelea kuupitia mkataba wa EPA, ambao ulipaswa kuwa umetiwa saini, October mosi mwaka huu.

Wakizungumza kwenye mahojiano na gazeti moja la nchini Rwanda la “The New Times”, wabunge hao wamesema kuwa mkataba huo ni hatari kwa viwanda vidogo vya ndani, ambavyo wamesema vinaweza kufa kutokana na mkataba huo.

Wabunge hao wamesema kuwa, kuna hatari kubwa ya viwanda vya ukanda na uchumi wake kutetereka na hivyo kutokuwa na ushindani ulio sawa na bidhaa zitakazokuwa zikitoka barani Ulaya.

Mmoja wa wabunge hao, Marie Arena kutoka bunge la Ulaya, amesema kuwa kwa namna mkataba huo ulivyo hivi sasa, hauna usawa na ikiwa utatekelezwa jinsi ulivyo, utahamasiaha mazingira yasiyokuwa ya ushindani.

Wamesema kuwa umoja wa Ulaya umekuwa ukiweka shinikizo kwa nchi wanachama kwakuwa iliamini nchi ya Kenya ingeweza kuzishawishi nchi nyingine kutia saini ili kulinda soko lake kwenye nchi za Ulaya.

“Nafikiri ni mkataba ambao hauna tija kwa nchi za Afrika Mashariki na ndio maana umoja huo umekuwa ukishinikiza utiwe saini ukiitumia Kenya kama kinara wa Jumuiya. Kenya ndio nchi pekee yenye maslahi na mkataba huo kwakuwa wao wamepiga hatua kuliko wengine. Wao Kenya wanataka mkataba huu utiwe zaini ili waendelee kuwa na soko Ulaya,” alisema mbunge huyo.

Awali kulikuwa na hofu kuwa ikiwa nchik hizi zisingekuwa zimetia saini mkataba huu hadi kufikia September 30 mwaka huu, basi nchik ya Kenya ingepoteza soko kwenye nchi za Ulaya, suala ambalo hata viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliligusia na kutaka wasishinikizwe.

Wabunge hawa wameongeza kuwa isingekuwa rahisi kwa nchi za ukanda kuzitoza kodi bidhaa kutoka Ulaya na kwamba hata viwanda vyake vya ndani vingekufa kwakuwa havina uwezo wa kushindana na vile vya Ulaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.