Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Agathon Rwasa ahofia usalama wake licha ya kuwa kiongozi bungeni

Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa alipozungumza na RFI tarehe Julai mwaka 2015 jijini Bujumbura
Kiongozi wa chama cha FNL Agathon Rwasa alipozungumza na RFI tarehe Julai mwaka 2015 jijini Bujumbura REUTERS/Mike Hutchings

Mwanasiasa wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa anaishutumu serikali nchini humo kwa kumwekea vikwazo vya kusafiri, kuwakamata na kuwasumbua wafuasi wake.

Matangazo ya kibiashara

Aimé Magera msemaji wa mwasiasa huyo anayeongoza chama cha upinzani cha FNL, amesema kiongozi wao amekuwa akipokea vitisho licha ya kuwa Naibu Spika katika  bunge la kitaifa.

Magera ameongeza kuwa Rwasa anahofia usalama wake huku  wafuasi wa chama cha FNL zaidi ya 200 wakiwa wamekamatwa tangu mwezi Januari mwaka huu na kuzuiwa katika maeneo yasiyofahamika bila hata kufunguliwa mashitaka.

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya wafausi wa FNL ambao wanaonekana kuwa waasi na hivyo maadui wa serikali, wameendelea kuhofia usalama wao nchini Burundi.

Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani nchini humo Thérence Ntahiraja, amekanusha madai hayo na kusema hayana msingi na kueleza kuwa ni ya kisiasa.

Ntahiraja amesema Rwasa anatumia mbinu hii kujitafutia umaarufu wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo na yale ya Kimataifa yamekuwa pia yakishutmu serikali ya Bujumbura kwa kuwakamata raia wasiokuwa na hatia na kuwazuia bila ya kuwafikisha Mahakamani.

Ukamataji huu umekuwa ukiendelea tangu jaribio la kumpindua rais Pierre Nkurunziza mwaka 2015.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.