Pata taarifa kuu
TANZANIA

Wizara yawataka wadau nchini TZ kusaidia kupatikana kwa msanii Roma Mkatoliki

Roma Mkatoliki, mwanamuziki aliyetekwa Tanzania
Roma Mkatoliki, mwanamuziki aliyetekwa Tanzania http://www.timesfm.co.tz

Wizara ya habari Utamaduni sanaa na Michezo nchini Tanzania imewaomba wadau mbalimbali na wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo mwanamuziki wa nyimbo za kizazi kipya Ibrahimu Musa al maarufu Roma Mkatoliki ambaye ametoweka tangu tarehe April 05 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Roma pamoja na wenzake wawili wanadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa studio jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kazi za muziki na hadi sasa bado hawajulikani walipo huku vyombo vya dola vikisema kuwa msanii huyo hashikiliwi katika kituo chohote cha polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo suala la kutoweka kwa mwanamuziki huyo  lina mwenendo wa jinai na hivyo wizara inawataka wananchi kushirikiana ili kumpata msanii huyo pamoja na wenzake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.