Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Odinga: Kenyatta acha kuitishia Mahakama Kuu

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amuonya Kenyatta kutoendelea kuitishia Mahakama Kuu.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amuonya Kenyatta kutoendelea kuitishia Mahakama Kuu. REUTERS/Thomas Mukoya

Kiongozi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuacha kuitisha Mahakama ya Juu baada ya ushindi wao kufutwa wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kampeni za siasa jijini Nairobi mwishoni mwa wiki kuelekea katika Uchaguzi mpya wa urais, Odinga amesema vitisho dhidi ya Mahakama na Jaji Mkuu Dvaid Maraga havikubaliki.

Hata hivyo, viongozi wa chama cha Jubilee wakiongozwa na Naibu rais William Ruto wameendelea kuikosoa Mahakama kwa uamuzi ambao wanasema ni kubadilisha uamuzi wa wananchi.

Mashirika ya kiraia nchini humo leo yanatarajiwa kuwa na kikao kulaani matamshi ya wanasiasa wa Jubilee dhidi ya Mahakama lakini pia kushinikiza kufanyiwa marekebisho ndani ya Tume ya Uchaguzi kabla ya uchaguzi mpya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.