Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Benjamin Mkapa akutana na wanasiasa wa Burundi walio uhamishoni

Mratibu katika mazungumzo ya Warundi Benjamin William Mkapa.
Mratibu katika mazungumzo ya Warundi Benjamin William Mkapa. EBRAHIM HAMID / AFP

Mratibu katika mazungumzo ya Warundi Benjamin William Mkapa amekutana hii leo jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania na ujumbe wa wawikishi wa muungano wa upinzani wa Burundi uishio uhamishoni Cnared.

Matangazo ya kibiashara

Lengo hasa ni kuangalia mchakato wa mazungumzo wapi umefikia na mbinu za kufufua upya mazungumzo hayo ambayo yatakuwa ya moja kwa moja baina ya upinzani na serikali.

Mazungumzo haya yanakuja ikiwa ni siku kadhaa baada ya msuluhishi kukutana na ujumbe wa serikali ya Burundi jijini Dar es salaam, ambapo pande hizo mbili zilikutana hivi karibuni nchini Helsinki

Naibu mwenyekiti wa Cnared Chauvineau Mugwengezo ameiambia dhaa ya Kiswahili ya RFI kwamba mazungumzo haya yanafanyika wakati kukikwa na mchakato wa uchaguzi nchini burundi ambao hautokuwa na tija, bila kukamilisha mazungumzo haya.

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi ulizuka baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu mwaka 2015.

Machafuko nchini Burundi yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki zabinadamu, na maelfu kukimbilia nje ya nchi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.