Pata taarifa kuu
KENYA-HRW-HAKI-USALAMA

HRW: Polisi ilihusika na vitendo viovu dhidi ya raia Kenya

Polisi katika mji wa Kisumu, Agosti 12, 2017, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Raila Odinga, mgombea wa urais aliejiondoa katika kinyang'anyiro hicho.
Polisi katika mji wa Kisumu, Agosti 12, 2017, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Raila Odinga, mgombea wa urais aliejiondoa katika kinyang'anyiro hicho. REUTERS/James Keyi

Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Human Rights Watch inalaani uhalifu wa kijinsia, uliofanywa na vikosi vya usalama, wakati wa uchaguzi wa Kenya mwaka mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hili liliendesha uchunguzi wake katika vitongoji vya Nairobi na Kisumu na Bungoma, magharibi mwa Kenya, katika ngome za upinzani.

Ripoti ya Human Rights Watch, inawatuhumu maafisa wa usalama nchini Kenya, kuwabaka, kuwapiga na kuwanyanyasa raia wakati wa kipindi cha kisiasa.

"Watu waliokua wakiendesha vitendo hivyo walikua wakivaa sare ya polisi. Maneno haya, ambayo yamekua yakirejea katika ushuhuda wa waathirika, yanathibitisha kuhusika kwa polisi katika vitendo viovu ikiwa ni pamoja na ubakaji katika ngome za upinzani. Kati ya wanawake 65 waliohojiwa, nusu yao wananyooshea kidole polisi.

Vitendo hivyo vilihusiana moja kwa moja na uchaguzi, kulingana na ripoti hiyo. Mwathirika mmoja amesema alibakwa mbele ya watoto zake, baada ya kukataa kusema kwamba anamuunga mkono rais Uhuru Kenyatta. Mwingine ameelezea kwamba alishambuliwa na watu ambao walikuwa wakisherehekea ushindi wa Uhuru Kenyatta mbele ya maofisa wa polisi.

Human Right Watch inalaani vikwazo vingi vinavyozuia waathirika kupata huduma na kuwafungulia mashitaka wahusika.

Human Rights Watch inadai kwamba wanawake na wasichana waliobakwa wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007, bado wanakabiliwa na matatizo ya kimwili, kiafya na kisaikolojia.

Pia ripoti hiyo inasema serikali ya Kenya haijatoa usaidizi wa kimsingi kuwasaidia waathiriwa hao.

Kulingana na ripoti hiyo, zaidi ya visa 900 vya ubakaji viliripotiwa wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007.

Tangu mkuanza kwa mgogoro nchini Kenya, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekua yakilaani ukatili unaofanywa na polisi. Watu zaidi ya 70 waliuawa katika makabiliano na polisi tangu uchaguzi wa kwanza wa urais mnamo mwezi Agosti 2017. Tuhuma ambazo serikali imeendela kukanusha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.