Pata taarifa kuu
KENYA-HUMAN RIGHTS WATCH

Human Rights Watch yalaani kuzimwa kwa mitambo ya Vyombo vya Habari nchini Kenya

Human Rights Watch
Human Rights Watch @google

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameishtumu serikali ya Kenya kwa kuzima mitambo ya vyombo vya Habari nchini humo na kuwanyima raia haki ya msingi, kufuatilia kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga kuwa rais wa watu.

Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch, inasema hatua hiyo ya serikali ya Kenya ni kuwanyima haki ya msingi raia wa nchi hiyo.

Tume ya Mawasiliano nchini humo imezima mitambo ya runinga kuu nchini humo NTV, Citizen TV , KTN News na redio kadaa ili kuwazuia Wakenya kufuatilia kilichokuwa kinachotokea wakati wa kuapishwa kwa Odinga.

Mtafiti wa Human Rights Watch barani Afrika Otsieno Namwaya amesema, hatua ya serikali imekwenda kinyume na haki ya kupata habari kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo na sheria za Kimataifa.

"Kenya inarudi nyuma katika harakati za kuheshimu haki za binadamu na rais Kenyatta ana jukumu la kuhakikisha kuwa, anabadilisha hili,” alisema Namwaya.

“Ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki za binadamu na inaharibu sifa ya Kenya kimataifa,” aliongeza.

Tume ya taifa ya kutetea haki za Binadamu KNCHR na Kamati ya Kimataifa ya kuwalinda wanahahabari (CPJ) wamelaani pia hatua hiyo ya serikali na kusema kuwa, haikubaliki.

Hatua ya serikali ya rais Uhuru Kenyatta, imerudisha nyuma haki na uhuru wa vyombo vya Habari nchini Kenya licha ya nchi hiyo kupata katiba mpya mwaka 2010.

Wiki iliyopita, ripoti zilieleza kuwa Wahariri waliagizwa kufika Ikulu jijini Nairobi na kuagizwa kutopeperusha matangazo hayo la sivyo wapokonywe leseni.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.