Pata taarifa kuu
MAFURIKO-TANZANIA-KENYA

Mafuriko yawaathiri wakaazi wa jiji la Dar es salaam, wanafunzi washindwa kwenda Shule

Athari ya mafuriko katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania April 16 2018
Athari ya mafuriko katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania April 16 2018 http://www.mwananchi.co.tz/

Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika jiji la kibiashara la Tanzania Dar es salaam kuanzia jana imesababisha mafuruko katika maeneo ya mabondeni.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wakaazi wa jiji hilo wamelazimika kusalia majumbani na kushindwa kuendelea na shughuli zao za kawaida wakiwemo.

Mabasi ya mwendo kasi, yanayowasafirisha abiria kutoka Kimara kuelekea eneo la Kibiashara Kariako na katikati mwa jiji, yamesitisha huduma zake baada ya barabara kujaa maji katika eneo la Jangwani.

Wanafunzi wengi wamesalia nyumbani, baada ya kushindwa kuondoka nyumbani kutokana na maeneo wanayoishi kujaa maji.

Hali kama hii pia inashuhudiwa katika miji kadhaa ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Waathiriwa wa mafuriko katika Kaunti ya Narok nchini Kenya wamekwama baada ya barabara kuu kuelekea jiji kuu la Nairobi kujaa maji.

Mataifa ya Afrika Mashariki yameendelea kukumbwa na miundo mbinu mibovu ambayo haiwezeshi kupita kwa maji na kuhatarisha maisha ya watu.

Watalaam wa utabiri wa hali ya hewa wameonya kuwa mvua huenda zikaendelea kushuhudiwa kwa siku kadhaa, na kutoa wito kwa wakaazi wa maeneo ya mabondeni kuhamia maeneo salama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.