Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya amani ya Burundi kufanyika Aprili 25

Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa
Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa EBRAHIM HAMID / AFP

Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi, anatarajia kuitisha kikao kipya cha mazungumzo baina ya wadau wa Burundi kuanzia Aprili 25 katika mji wa Entebbe, nchini Uganda.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la mazungumzo hayo ni kujaribu kupata mkataba kwa mgogoro kabla ya kura ya maoni kuhusu mageuzi ya Katiba liopangwa kufanyika Mei 17 nchini Burundi.

Siku ya Jumatatu Aprili 16, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa walitoa taarifa ya pamoja kulaani msimamo wa Bujumbura kukataa kushiriki mazungumzo hayo, kabla ya kuifuta.

Taarifa ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa haikuwa wazi. Taasisi hizi mbili hazikuficha "wasiwasi" wao kuhusu uamuzi wa serikali ya Bujumbura wa kusimamisha ushiriki wake katika mazungumzo ya kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro unaoendelea.

Taarifa hiyo"ilikua inasisitiza" serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kuangalia upya msimamo wake haraka iwezekanavyo, kwa sababu inatakiwa kuchukua hatua haraka kujaribu kuokoa mkataba wa amani wa Burundi, uliyosainiwa Arusha mwaka 2000. Kufutwa kwa mkataba huo kuna hatari ya kutokea machafuko makubwa, kulingana na taarifa hiyo. Serikali inapanga kuandaa kura ya maoni kuhusu mageuzi ya Katiba mnamo Mei 17, katiba ambayo itamruhusu Rais Nkurunziza kusalia mamlakani hadi mwaka 2034. Jumuiya ya kimataifa inabaini kwamba Katiba mpya itaangamiza moja kwa moja mkataba huo ambao ulifungua njia ya kupatikana amani kwa miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa waliapa "kutekeleza jukumu lao kikamilifu" kama "wadhamini wa mkataba wa amani wa Arusha," bila kutoa maelezo zaidi.

Haijajulikana kuwa taarifa hiyo ilifutwa kwenye tovuti ya Tume ya Umoja wa Afrika kutokana na tatizo la kiufundi au lilifutwa kwa makusudi. Taarifa hiyo iliondolewa kwenye tovuti ya Tume ya Umoja wa Afrika mapema Jumatatu alasiri. "Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu hatua hiyo," alisema mwanadiplomasia wa Afrika mjini Addis Ababa.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa hawataki kuichukiza serikali ya Bujumbura. Bado wanatarajia kuokoa kile kinachochukuliwa kuwa mazungumzo ya mwisho ya wiki ijayo huko Entebbe, nchini Uganda.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.