Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-USHIRIKIANO

Macron aunga mkono Rwanda kuwania kwenye uenyekiti wa Francophonie

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenyeji wake Emmanuel Macron, katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Elysee, Mei 23, 2018.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenyeji wake Emmanuel Macron, katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Elysee, Mei 23, 2018. Francois Mori/Pool via Reuters

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameunga mkono Rwanda kuwani kwenye nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya nci zinazozungumza Kifaransa "Francophonie” (OIF). Hatu hii imekuja baada ya Rais Paul Kagame wa Rwanda kuzuru Ufaransa Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Rwanda Paul Kagame alipokelewa siku ya Jumatano Jumatano, Mei 23 alasiri na mwenyeji wake Emmanuel Macron kwa chakula cha mchana pamoja na wadau zaidi ya sitini wanaoongoza katika masuala ya dijitali.

Wawili hawa walikutana pia kwa mazungumzo. Mkutano ambao ulifuatiwa na mkutano na waandishi wa habari wakati ambapo Rais wa Ufaransa alitangaza kwamba anaunga Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kuwania kwenye nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa "Francophonie" (OIF).

Emmanuel Macron ana "imani" ambayo pia hakuweza kuificha: "Ikiwa kuna mgombea wa Afrika kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Francophonie, mgombea huyo atapewa nafasi kubwa. Ikiwa mgombea huu ni kutoka Afrika na ni mwanamke, hakuna saha kumpa nafasi kubwa ya kuwania. Kwa hiyo ninaamini kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda ana ujuzi na majukumu yote ya kufanya kazi hii, "alisema rais wa Ufaransa, akibainisha kuwa Louise Mushikiwabo ana" uzoefu kamili wa lugha ya Kifaransa. "

Uungwaji huu mkono kwa mgombea wa Rwanda kwenye nafasi hii ni ishara kubwa ambayo Ufaransa imeonyesha kwa nchi ya Rwanda. Emmanuel Macron amesema katika, kwa vitendo anataka kuonyesha nia yake ya kufufua uhusiano kamili na Rwanda.

Rwanda ni mwanachama wa Francophonie. Baadhi walifikia hata kuamini kwamba tulijitoa katika jumuiya hiyo, lakini sivyo. Tulijiunga na jumuiya nyingine, lakini sisi bado ni mwanachama wa Francophoni, amesema rais Paul Kagame.

Uungwaji huu mkono wa Ufaransa kwa Rwanda unaweza kuzua utata. Kwa sababu ya uhusiano mgumu kati ya Paris na Kigali tangu mwaka 1994, lakini pia kwa sababu Rwanda ilijiunga na Jumuiya ya Madola mwaka 2009, wakati ambapo Kiingereza kiliwekwa kama lugha rasmi nchini humo.

Lakini hii siyo tatizo kwa mujibu wa Rais Macron, ambaye Rwanda bado ni nchi inayozungumza Kifaransa, kabla ya kuongeza kwamba wazo lake ni kufikiri Francophonie katika lugha mbalimbali, akisisitiza kuunga mkono Rwanda kuwania kwenye nafasi hiyo.

"Nadhani Francophonie haiko katika vita na Jumuiya ya Madola au Kifaransa kuwa katika vita na Kiingereza. Badala yake, nadhani Francophonie ni sehemu ya ulimwengu ambapo kunazungumzwa lugha nyingi, hali ambayo inashuhudiwa katika nchi yangu. Hiyo haizui mpango uliopo kwa Francophonie, " amesema Louise Mushikiwabo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda.

Wakati huo huo Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenyeji wake Emmanuel Macron wamekubaliana nchi zao kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto ambazo zinalikabili bara la Afrika.

Miongoni mwa masuala ambayo viongozi hawa wamekubaliana kushirikiana ni pamoja na masuala ya usalama, biashara na teknolojia, huku rais Kagame akiitaka Ufaransa kuendelea kushirikiana na umoja wa Afrika kuondoa vikwazo vilivyopo sasa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.