Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-BIASHARA-MIRADI

AFD: Tumetoa Euro milioni 600 kuchangia maendeleo Tanzania

Watendaji wa AFD wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Remy Rioux pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Maendeleo Aghakan Dakta Gijs Walreven wakipokea maelezo ya ujenzi wa jengo jipya la Hospitali hiyo
Watendaji wa AFD wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Remy Rioux pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Maendeleo Aghakan Dakta Gijs Walreven wakipokea maelezo ya ujenzi wa jengo jipya la Hospitali hiyo Benazir Karim/Aghakan

Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD limetumia zaidi ya Euro Milioni 600 kuisaidia Tanzania kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka kumi ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na idhaa hii jijini Dar es salaam wakati akiwa katika ziara ya siku mbili nchini Tanzania Mkuu wa AFD, Rémy Rioux amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa umekuwa na manufaa katika sekta mbalimbali.

"Tunafadhili katika maeneo mengi miradi ya maji na umwagiliaji katika ziwa victoria na kukabiliana na uchafuzi wa Mazingira, katika afya,elimu hata katika usafiri" alisema Rioux.

Kwa upande Mwingine, Rioux amesema licha ya mafanikio hayo bado kuna changamoto za kufanyiwa kazi na washirika ili misaada inayotolewa iwe na matokeo chanya kwa walengwa.

Miongoni mwa sekta zinazonufaida na misaada kutoka shirika hilo ni pamoja na sekta ya afya nchini humo ambapo Hospitali ya Aghakan ni moja wapo, Dakta Gijs Walreven ni Mkurugenzi wa afya wa Hospitali hiyo.

"tumekuwa na ushirikiano na AFD kwa muda mrefu na ndio walitusaidia kujenga hospitali hii,sasa tunahitaji ushirikiano zaidi na wadau wengine wa afya katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali kama saratani na Kisukari na pia kupata elimu zaidi kwa wataalam wetu" alisema Walreven.

Shirika la AFD limekuwa na ushirikiano na Tanzania kwa miaka kumi ,sasa ziara hii ilihitishwa kwa kukutana na Mawaziri mbalimbali jijini Dodoma.

Ripoti ya mwandishi wa Rfi Kiswahili Steven Mumbi kutoka Dar es salaam.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.