Pata taarifa kuu
RWANDA-INDIA-MSUMBIJI-USHIRIKIANO

Rwanda kuwapokea viongozi kutoka Msumbiji, China, na India

Mjini kati Kigali, Rwanda
Mjini kati Kigali, Rwanda RFI/Stéphanie Aglietti

Rwanda wiki hii na wiki ijayo, itakuwa mwenyeji wa wageni mashuhuri kutoka Msumbiji, China na India. Viongozi wa China pia watazuru nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Mauritius.

Matangazo ya kibiashara

Tayari rais wa Msumbiji Filipe Nyusi yupo nchini humo kwa ziara ya siku tatu na atafuatiwa na rais wa China Xi Jinping, atakayekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kuzuru Rwanda.

Baadaye kati ya tarehe 23-24 mwezi huu Waziri Mkuu wa India Nahedra Modi atakuwa jijini Kigali.

Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu ushirikiano wa Rwanda na bara la Afrika kuhusu masuala mbalimbali hasa biashara na usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.