Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Mazungumzo mapya ya kisiasa ya Warundi yaahirishwa

Polisi wa Burundi wakiendelea kupiga doria katika mitaambalimbali ya mji wa Bujumbura.
Polisi wa Burundi wakiendelea kupiga doria katika mitaambalimbali ya mji wa Bujumbura. AFP PHOTO / SIMON MAINA

Mazungumzo mapya ya kisiasa ya Warundi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kati ya tarehe 19 na 24 mwezi huu mjini Arusha nchini Tanzania, yameahirishwa.

Matangazo ya kibiashara

Macocha Moshe Tembele, Msaidizi wa kiongozi wa mpatanishi katika mazungumzo haya rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa amesema sababu ya kuahirishwa kwa mazungumzo haya nni kwa sababu Burundi itakuwa inaadhimisha miaka 25 tangu kuuawa kwa rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia Melchior Ndadaye.

Mazungumzo haya yanatarajiwa kuleta mwafaka wa kisiasa baada ya jaribio la mapinduzi mwaka 2015 na rais Piere Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Hakuna mwafaka wowote uliowahi kupatikana katika mazungumzo yaliyopita.

Mashirika kadhaa ya kiraia yanaona kuwa mzungumzo hayo yajayo hayatakuwa suluhu ya mzozo uliopo ukizingatia kuwa serikali ya Burundi bado hainaonyesha umuhimu wa kuzungumza na wapinzani wake.

Serikali ya Burundi imekuwa ikipinga kuketi kwenye meza ya mazungumzo na wanasiasa hao kutoka Cnared ikiwashtumu kwamba baadhi yao walihusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuliwa Mei 15, 2015.

Machafuko nchini Burundi yamesababisha zaidi ya watu 2000 kuawa kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu nchini Burundi na maefu kadhaa kutoroka makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.