Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya mwisho baina ya Warundi kufanyika Jumatano Arusha

Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015.
Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015. © AP

Mpatanishi wa amani ya Burundi, rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Jumatano ya wiki hii anatarajiwa kuzikutanisha pande zinazohasimiana jijini Arusha Tanzania, katika mazungumzo ambayo yanatajwa huenda yakawa ni ya mwisho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

ais wa zamani wa Tanzania William Mkapa alipewa wadhifa kusimamia mazungumzo ya amani katika mzozo unaokabili Burundi tangu mwaka 2015 kutoka kwa rais Yoweri Museveni.

Katiba iliosainiwa mwaka 2000 inasema kuwa rais anaruhusa kugombea kiti cha urais kwa mihula miwili.

Mazungumzo haya yanatarajiwa kujikita katika kusaka muafaka kuhusu namna bora itakayosadia pande hizo kushiriki kwa uhuru na uwazi katika maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Mazungumzo haya ambayo yalianza tangu mwezi Desemba mwaka 2015, baada rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula watatu na kusababisha vurugu, yameshindwa kutoa majibu ya hatma ya taifa hilo ambalo limeshuhudia maelfu ya raia wake wakikimbilia katika nchi jirani.

Ripoti zinasema kuwa watu zaidi ya 2,000 wamefariki nchini Burundi tangu kuzuka kwa mzozo huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.