Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Rwanda: Ofisi ya mashtaka kukata rufaa dhidi ya kuachiliwa huru Diane Rwigara

Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Shima Rwigara mbele ya waandishi wa habari mjini Kigali, Rwanda, Juni 20, 2017.
Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Shima Rwigara mbele ya waandishi wa habari mjini Kigali, Rwanda, Juni 20, 2017. © REUTERS

Mwanasheria Mkuu wa Rwanda, Jean Bosco Mutangana, ametangaza mbele ya waandishi wa habari kwamba atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa Desemba 6 ulio muachilia huru mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa rais Paul Kagame, Diane Rwigara na mama yake.

Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka 22 kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

"Upande wa Mashitaka hauridhishwi na uamuzi wa mahakam. Kwa hiyo tumeamua kukata rufaa katika siku zijazo," Bw Mutangana amesema katika mkutano na waandishi habari mjini Kigali."

Tulisoma kwa makini uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Rwigara na tumeamua kukata rufaa (...) Tunaamini kwamba ushahidi ambao tuliwasilisha mbele ya Mahakama ya juu haukuzingatiwa kikamilifu, "Jean Bosco Mutangana ameongeza.

Mapema mwezi Desemba, Diane Rwigara, mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, aliachiliwa huru baada ya kufutiwa makosa yaliyokuwa yanamkabili yeye na mama yake Adeline Rwigara.

Mahakama Kuu ya Rwanda ilitangaza kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote.

Katika uamuzi wake, Mahakama Kuu ya Rwanda ilibaini kwamba ukosoaji wa Diane Rwigara dhidi ya serikali, hasa katika mikutano na waandishi wa habari, haikuwa "kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi" kwa sababu ilikuwa haki yake katika uhuru wa kujieleza anayopewa na Katiba ya Rwanda na sheria za kimataifa.

Majaji pia walibaini kwamba upande wa mashtaka haujaonyesha kwamba Diane Rwigara alighushi anyaraka alipowasilisha fomu yake ya uchaguzi kwa tume ya uchaguzi kwa kushiriki katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017. Uamuzi wa kukataliwa kwa Diane Rwigara kuwania katika uchaguzi huo ulikosolewa na serikali za magharibi na mashirika ya haki za binadamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.