Pata taarifa kuu
UGANDA-BOBI-SIASA

Mwanamuziki Bobi Wine akimbilia mafichoni

Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la usanii Bobi Wine, wakati akionekana mbele ya umati wa watu Kibera, Nairobi, alipokuwa katika ziaraya siku tano nchini Kenya.
Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la usanii Bobi Wine, wakati akionekana mbele ya umati wa watu Kibera, Nairobi, alipokuwa katika ziaraya siku tano nchini Kenya. © AFP

Mwanamuziki maarufu na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi anayefahamika kwa jina la Bobi Wine ameamua kukimbilia mafichoni baada ya kutafutwa na polisi ya Uganda katika hoteli alipokuwa anaishi, wakili wake amesema.

Matangazo ya kibiashara

Bobi Wine alitarajiwa kufanya tamasha la muziki siku ya Jumamosi katika mji wa Jinja, kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala, wakati polisi iliendesha msako katika hoteli yake.

Bobi Wine "alilazimika kukimbilia mafichoni," huku ndugu zake na marafiki zake wa karibu wakikamatwa na kupigwa, amesema Robert Amsterdam, mwanasheria wa Bobi Wine mwenye makazi yake mjini London.

"Polisi walivamia hoteli ambapo tulikuwa tumepumzika kabla ya tamasha la usiku wa leo na kuwatia mbaroni baadhi ya wajumbe wa timu yetu. wakati huu tunapoongea, polisi imezingira eneo lote kwa kunisaka, "Bobi Wine ameandikja kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mwanasheria wa nyota huyo maarufu wa kizazi kipya ametaja operesheni hiyo ya polisi kama "kitendo cha aibu cha ukandamizaji wa kisiasa kinachofanywa na serikali ya Uganda kwa kukiuka haki za binadamu za Bobi Wine".

Tangu alipotangaza mwaka 2017 kama mpinzani na mkosoaji mkuu wa Rais Yoweri Museveni, mamlaka mara kwa mara imeamua kumzuia Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 36, kuonekana mbele ya umati wa watu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.