Pata taarifa kuu
BURUNDI-NKURUNZIZA-SIASA-KESI

Wasichana watatu wazuiwa jela kwa kuchorachora picha ya rais Nkurunziza

Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana

Wasichana watatu nchini Burundi, wamezuiwa jela wakisubiri kuhukumiwa Mahakamani baada ya kufutafuta picha ya rais Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vya kusoma.

Matangazo ya kibiashara

Imeelezwa kuwa wasichana hao wana umri wa miaka 15, 16 na 17 na iwapo watapatikana na kosa la kumdhihaki rais, atafungwa jela miaka mitano.

Majaji wamesema kuwa wasichana hao ni lazima wafunguliwe mashtaka kwa kosa hilo, na kuagiza wazuiwe kwenye jela ya watoto mjini Ngozi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Muungano wa mashirika ya kiraia 48 FENADEB, yamelaani hatua hiyo na kusema haikubaliki na ni ukiukwaji wa haki za watoto.

Wasichana hao wamekuwa wakizuiwa tangu tarehe 12 mwezi Machi, baada ya kukamatwa pamoja na mvulana mwenye umri wa miaka 13 ambaye baadaye aliachiliwa huru.

Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali ndio inayoshughulikia kesi hii, na haijafahamika ni lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa mujibu wa Lewis Mudge, mwanaharakati kutoka Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la  Human Rights Watch.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.