Pata taarifa kuu
UGANDA-KENYA-USHIRIKIANO

Rais wa Uganda Museveni azuru Kenya

Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta (kulia).
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta (kulia). State House Kenya/twitter.com

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni anazuru Kenya kwa ziara ya siku mbili. Aliwasili Jumatano wiki hii, na kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Mombasa, Pwani ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wamezungumzia masuala ya biashara kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki, wakati huu Uganda ikiendelea kuvutana na Rwanda kuhusu masuala ya kibiashara.

Leo Alhamisi anatarajia kuzuru bandari ya Mombasa ambayo Uganda inatumia kupokea idadi kubwa ya mizigo yake na baadaye yeye pamoja na rais Uhuru Kenyatta wanatarajia kuabiri treni ya mwendo kasi kutoka Mombasa hadi jijini Nairobi.

Katika hatua nyingine, rais Kenyatta amesema amekubaliana na mwenzake kuhusu namna ya kutatua mzozo wa kisiwa cha Migongona na namna ya kunufaika na maji ya Ziwa Victoria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.