Pata taarifa kuu
BURUNDI-HAKI

Wanafunzi walioharibu picha ya rais waachiliwa huru Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. REUTERS/Evrard Ngendakumana

Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu nchini Burundi wamepongeza hatua ya Wizara ya Sheria nchini humo kutangaza kuwaacha huru wasichana watatu wa shule ya msingi wanaozuiliwa jela kwa kosa la kuharibu picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wanaharakati wamesema wanashangazwa kuona baada ya kutangazwa kwa hatuwa hiyo wasichana hao bado wamesalia korokoroni wakati ambapo walitakiwa kuachiwa muda huo huo baada ya kutangazwa.

Waziri wa sheria nchini Burundi Aime Laurentine Kanyana amewataka wazazi kuimarisha malezi kwa watoto wao.

Mashirika ya kutetea haki za watoto nchini Burundi yameshauri uchunguzi wa kina ufanyikekabla ya kuwatia watoto hao hatiani ili kubaini ni kwa nini matukio kama hayo yanajitokeza.

Wasichana hao wenye umri wa miaka 15, 16,na 17 wanaosoma shule moja ya sekondari darasa la saba kaskazini mwa Burundi, wamekuwa kizuwizini kwa siku kadhaa. Walipatikana na hatia ya kuchafua picha ya rais Pierre Nkurunziza wa Burundi iliyo kwenye vitabu vyao vya shule.

Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa Kirundi, kaskazini mwa Burundi, machi 12, 2019

Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.

Mapema wiki hii makundi ya haki za binadamu yalituma vibonzo vinavyoonyesha picha ya Nkurunziza iliyochafuliwa kwa michoro kwenye kurasa za mtandao wa twitter, kuonyesha kuwa wanapinga kukamatwa kwa watoto hao wa shule.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.