Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA

Mwanamuziki nguli na mbunge wa upinzani Bobi Wine akamatwa Uganda

Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano, Kampala Julai 11, 2018.
Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano, Kampala Julai 11, 2018. Isaac Kasamani / AFP

Mwanamuziki maaarufu nchini Uganda na mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi anayejulikana kwa jina maarufu la Bobi Wine amekamatwa baada ya kukabiliana na vikosi vya usalama alipokuwa akijielekeza kufunguwa tamasha lake la muziki la siku kuu ya pasaka, tamasha ambalo lilipigwa marufuku na mamlaka nchini Uganda.

Matangazo ya kibiashara

Purukushani hizo zilitokea baada ya maafisa wa polisi kuuzuia msafara uliokuwa ukiongozwa na Bobi wine katika tamasha lake la One Love katika eneo la Busabala, kwa mujibu wa chanzo cha polisi ambacho hakikutaja jina lake.

Kwa mujibu wa chanzo hicho waandalizi wa tamasha hilo pia wamekamatwa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Makindye Magharibi, Allan Ssewanyana, kulingana na gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mashahidi Bobi Wine alikamatwa na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa eneo lisilojulikana, lakini mwanamuziki Nubian Li ambaye alikuwa akiongozana naye katika gari moja hakukamatwa.

Hivi karibuni rais Yoweri Kaguta Museveni alionya kwamba katika siku zijazo hakuna mtu atakayefidiwa kwa matamasha ambayo yamepigwa marufuku kutokana na siasa, huku akibaini kwamba hatokubali matamasha ya muziki uliojaa siasa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.