Pata taarifa kuu
KENYA-WAKIMBIZI-MAPENZI-JINSIA-MOJA-KAMBI

Wakimbizi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja warudishwa kambini nchini Kenya

Bendera inayotumiwa na wapenzi wa jinsia moja
Bendera inayotumiwa na wapenzi wa jinsia moja Justin Powell/Wikimedia Commons

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi UNHCR, inasema itatoa msaada wa kuwalinda watu wakimbizi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambao wamerudishwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la wanaume 76, wanawake na watoto walikuwa wanaishi jijini Nairobi lakini wamekuwa wakilengwa kwa sababu ya vitendo vyao na sasa wameamua kurudi kambini.

Siku ya Jumatano, bila ya kupewa taarifa yoyote, mabasi mawili yaliwasili walikokuwa wanaishi ili kuwasafirisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma.

Tume ya UNHCR, imesema kuwa itawapa ushauri na kuwasaidia watu hao. Wakimbizi wengi wanaoishi katika kambi hiyo wanatokea nchini Sudan Kusini, DRC, Burundi na Somalia.

Mapenzi na vitendo vya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Kenya, na anayepatikana na kosa hilo, anafungwa jela hadi miaka 14.

Hivi karibuni, Mahakama ilisisitiza kuwa ni kinyume cha sheria kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.