Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Wabunge wanawake watishia kushiriki vikao vya bunge na wanao wachanga Kenya

Makao makuu ya Bunge la Kenya.
Makao makuu ya Bunge la Kenya. © Photo: Rotsee2, source: Wikipédia

Wabunge wanawake wenye watoto nchini Kenya wametishia kuja na watoto wao kwenye vikao vya bunge, kushinikiza kutengewa eneo maalum ya kunyonyesha wanao, wanapokuwa kazini, baada ya mbunge mwenzao kuondolewa kwenye vikao vya bunge baada ya kuja na mwanaye mchanga.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wametishia kuchukua hatua hiyo, baada ya mbunge mwenzao Zuleika Hassan kufukuzwa bungeni baada ya kuhudhuria vikao vya bunge na mwanaye mchanga.

Kitendo hicho, kilizua mvutano katika bunge hilo jijini Nairobi, huku Spika akipata wakati mgumu kuwatuliza wabunge waliotofautiana na hatua ya mbunge huyo kuondolewa bungeni.

Kiongozi wa chama tawala bungeni Aden Duale, alikuwa miongoni mwa wabunge waliounga mkono hatua ya Spika kumwondoa mbunge huyo.

Alipoulizwa, mbunge huyo alisema hakuwa na mtu wa kumwachia mwanaye, lakini pia akaeleza kuwa anatekeleza kupitishwa kwa sheria kuwa wabunge wa kike wenye watoto wanaweza kuja na wanao bungeni na kuwanyonyesha.

Tukio hili limetokea wakati Kenya ikijiunga na mataifa mengine ya Afrika kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji watoto wachanga.

Licha ya Kenya kupitisha sheria kuruhsu wanawake wenye watoto kuwanyonyesha wanao katika maeneo ya kazi, bungeni, hakuna jengo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuwasadia wabunge wa kike wenye watoto wanaonyonya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.