Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Burundi: Mwili wa albino aliyeuawa wapatikana

Watoto wwenye ulemavu wa ngozi wako hatarini katika nchi nyingi za Afrika.
Watoto wwenye ulemavu wa ngozi wako hatarini katika nchi nyingi za Afrika. TONY KARUMBA / AFP

Visa vya mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi vimeanza tena kuripotiwa nchini Burundi, huku raia wakilauamu vyombo vya usalama kutowajibika kwa kazi yao hasa kukomesha vitendo hivyo viovu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika linalotetea haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Maalbino) nchini Burundi, mwili wa albino kijana aliyetoweka, ulipatikana Jumamosi, Agosti 17 Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo.

Mwili wa Bonheur Niyonkuru, kijana wa miaka 15, ulipatikana Jumamosi usiku Kaskazini-Magharibi mwa nchi, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mkoa wa Cibitoke. Taarifa za kupotea kwa kijana huyo zilianaza kutolewa Jumanne usiku.

Tangu mwaka 2008, karibu watu zaidi ya 20 wenye ulemavu wa nguzi (maalbino) wameuawa nchini Burundi.

Kwa mujibu wa Kazungu Kassim, kiongozi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, tukio la mwisho la kuuawa kwa albino lilitokea mnamo mwaka 2016. Lakini mtoto wa miaka 4 mwenye vinasaba vya ualbino alitoweka tangu mwezi Oktoba 2018 katika wilaya ya Cendajuri, mkoani Cankuzo, karibu na mpaka na Tanzania.

Mtoto huyo alipatikana amekufa, na baadhi ya viungo vya mwili wake vilikosekana. Mguu mmoja na mkono wa kulia vilikatwa, pamoja na ulimi.

Katika nchi zingine za Kiafrika, watu wenye ulemavu wa ngozi wanawindwa, kuuawa na kukatwa baadhi ya viungo, kisha hutumiwa katika imani za kishirikina.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.