Pata taarifa kuu
BURUNDI-CNL-SIASA-USALAMA

Burundi: Mwanaharakati wa chama cha upinzani auawa katika shambulio

Tukio hilo lilitokea kama kilomita kumi na tano kutoka Muyinga, kaskazini mashariki mwa Burundi.
Tukio hilo lilitokea kama kilomita kumi na tano kutoka Muyinga, kaskazini mashariki mwa Burundi. © Google Maps

Chama kikuu cha upinzaji nchini Burundi cha CNL, kimeelezea kifo cha mmoja wa wafuasi wake, na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio lililotokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, Agosti 19.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chama cha CNL, tukio hilo lilitokea kama kilomita kumi na tano kutoka katikati mwa mji wa Muyinga, Kaskazini Mashariki mwa Burundi, ambapo wafuasi zaidi ya 300 walikuwa wamekusanyika kwa mkutano. Walishambuliwa wakiwa njiani wakirudi makwao na watu waliojihami kwa mapanga.

Kiongozi wa chama cha CNL, Agathon Rwasa, ameshtumu vijana wkutoka chama madarakani, CNDD-FDD, Imbonerakure, kuhusika na shambulio hilo, na kuwanyooshea kidole cha lawama viongozi kwamba wanahusika na tukio hilo. "Walipokosa usafiri, waliamua kulala kwenye makao makuu ya chama cha CNL katika Mkoa wa Muyinga, lakini polisi iliwakatalia," Bw Rwasa amesema. Agathon Rwasa amebaini kwamba, Mkuu wa polisi katika Mkoa wa Muyinga aliwatimuwa katika mji wa Muyinga "kama wahalifu wasio kuwa kawaida".

"Walipofika kilomita zaidi ya kumi kutoka Muyinga, walishambuliwa na watu waliojihami kwa mapanga. Mtu mmoja alifariki papo hapo kutokana na majeraha aliyopata na wengine saba wamelazwa hospitali mkoani Muyinga, " Agathon Rwasa ameongeza.

Katika siku za hivi karibuni, chama cha CNL kimekuwa kikilaani vitendo vya mara kwa mara vya udhalilishaji na vitisho kwa wanasiasa na wafuasi wa upinzani. Chama hicho kinabaini kwamba ofisi zake 18 zimeharibiwa katika miezi miwili iliyopita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.