Pata taarifa kuu
RWANDA-UGANDA-USHIRIKIANO

Yoweri Museveni na Paul Kagame waahidi kukomesha mgogoro baina ya nchi zao

Rais wa Angola Joao Lourenço akizungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusaini makubaliano ya amani ya kumaliza uhasama kati ya Rwanda na Uganda, Agosti 21, 2019.
Rais wa Angola Joao Lourenço akizungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kusaini makubaliano ya amani ya kumaliza uhasama kati ya Rwanda na Uganda, Agosti 21, 2019. © JOAO DE FATIMA / AFP

Marais wa Rwanda na Uganda wamefikia makubaliano ya kumaliza uhasama ulio kuepo kati ya nchi hizi mbili jirani. Paul Kagame na Yoweri Kaguta Museveni wametia saini mkataba wa amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe ya kutia saini mkataba huo zimehudhuriwa na marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Angola na Congo Brazzaville.

Felix Tshisekedi, João Lourenço na Denis Sassou Ngueso wamefanya kazi kubwa kwa kuwapatanisa wawili hao katika mgogoro huo uliokuwa ukiendelea kati ya Rwanda na Uganda.

Mgogoro kati ya nchi hizi mbili umekuwa ukiendelea kwa miaka mitatu sasa, na umekandamiza maisha ya raia kutoka nchi hizi hasa wale wa mpakani.

Chanzo cha mgogoro

Rwanda imekuwa ikishtumu Uganda kushirikiana na waasi wanaoongozwa na Kayumba Nyamwasa na kundi lake RNC kuhatarisha usalama wake, huku ikinyooshea kidole cha lawama serikali ya Kampala kula njama na waasi hao kwa kuwafunga na kuwatesa raia wake.

Hata hivyo Uganda imekuwa ikishtumu serikali ya Kigali kuwatum abaadhi ya maafisa wake kufanya ujasusi katika aridhi yake.

“Tumekubaliana kumaliza tofauti zetu na tumefikia hatua kubwa ya kutia saiuni mkataba wa amani. Tunahakikishi raia wetu kwamba kuanzia sasa tunajianda kufungua mpaka uliokuwa umefungwa na kushughulikia masuala mengine nyeti, “rais Paul Kagame amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Angola.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.