Pata taarifa kuu
TANZANIA-UHURU WA HABARI

Jamii Forums yatunukiwa tuzo ya habari ya Daud Mwangosi

Mkurugenzi wa Jamii Forums Maxence Melo akionyesha tuzo aliyotunukiwa huko visiwani Zanzibar leo Septemba 6 mwaka 2019
Mkurugenzi wa Jamii Forums Maxence Melo akionyesha tuzo aliyotunukiwa huko visiwani Zanzibar leo Septemba 6 mwaka 2019 Jamii Forums/Twitter

Mtandao mashuhuri wa Jamii Forums umetunikiwa tuzo ya kutetea kazi ya habari ya Daud Mwangosi. 

Matangazo ya kibiashara

Tuzo hiyo imetolewa leo na taasisi ya klabu ya waandishi wa habari tanzania (TPC), ambayo imefanyika visiwani Zanzibar asubuhi hii.

Tuzo ya Daud Mwangosi hutolewa kila mwaka kwa mwanahabari au taasisi ya habari inayofanya kazi ya kuimarisha uhuru wa habari na kujieleza nchini Tanzania.

Tuzo hiyo hutolewa ikiwa ni kumbukumbu ya mwanahabari Daud Mwangosi aliyeuawa mwaka 2012 kwa kupigwa bomu wakati akiripoti mkutano wa kisiasa huko Iringa, Kusini magharibi mwa Tanzania.

Hii ni tuzo ya pili kwa Jamii Forums kutunikiwa ambapo baadaye mwezi Novemba Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums Maxence Melo atatunukiwa tuzo ya kimataifa ya kutetea uhuru wa habari huko Washington nchini Marekani.

Jamii Forums iliyoasisiwa zaidi ya miaka kumi iliyopita imejizolea umaarufu kwa kuwa mtandao unaofichua maovu yakiwemo ya rushwa na ufisadi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.