Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA

Ufaransa kutekeleza Mradi wa kuitunza Theluji ya Mlima Kilimanjaro

Kibo Summit of Kilimanjaro
Kibo Summit of Kilimanjaro Chris 73/Wikimedia Commons

Mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kuyeyuka kwa theruji katika milima mbalimbali Dunia hatua inayoisukuma nchi ya Ufaransa kuja na mradi wa kufanya utafiti ili kuhifadhi barafu unaoitwa Kumbukumbu ya Barafu iliyopo katika Mlima mrefu barani Afrika wa Kilimanjaro.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia mradi huo Jijini Dar es salaam, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema lengo ni kuchukua sampuli na kufanya utafiti ili kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi barafu pekee iliyosalia barani Afrika ambayo ipo katika mlima huo.

Hatua inayofuata sasa katika mradi huu wa kimataifa ni kujikita katika theruji pekee iliyosalia barani Afrika ambayo iko katika mlima Kilimanjaro. Katika mradi huu unalenga kunufaisha pande zote mbili,ambao utaundwa na wadau wote nchini Tanzania, wakiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala wa Taifa kama TANAPA. TAWIRI, TAFORI, TFS, TMA, COSTECH na Vyuo vikuu: UDSM, SOKOINE, na Chuo cha Nelson Mandela” alisema Clavier

Pia utafiti huo unalenga kubaini endapo Juhudi hazitafanyika kuhifadhi Mazingira kutakua na athari gani kimazingira na theruji hiyo itakuwepo kwa miaka mingapi. Dakta Ezekiel Mwakalukwa ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Malia asili na Utalii amesema serikali imeanza kuchukua hatua na ipo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuitunza Theruji iliyopo.

Mradi wa Kimataifa wa kumbukumbu ya saruji ulianzishwa mwaka 2015 na safari ya kwanza ilianzia nchini Ufaransa katika milima yenye barafu (theruji) ya Alpes, na kufuatiwa na safari nyingine mwaka 2017 nchini Bolivia kwenye theruji, na mwaka 2018 safari hiyo ilielekea nchini nchini Urusi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.