Pata taarifa kuu
UN-TANZANIA-HADZA-MAZINGIRA

Umoja wa Mataifa waituza Jamii ya Hadza nchini Tanzania kwa kutunza mazingira

Ezekiel Philipo kiongozi wa jamii ya
Ezekiel Philipo kiongozi wa jamii ya en.rfi.fr

Jamii ndogo  ya Hadza inayoishi msituni na kujihusisha na uwindaji na kuhamahama nchini Tanzania imepata tuzo ya Umoja wa Mataifa kutokana na jitihada zao za kutumia njia za kiasili kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko hali ya hewa.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miaka 40,000 jamii ya Hadza imekuwa ikiishi katika bonde la Yaeda, Kusini mwa Ikweta kati ya Ziwa Esayi na Mlima Ngorongoro, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Jamii hiyo imetuzwa Euro 300,000 kutokana na juhudi zao za kiasili za kutunza mazingira, wakati huu dunia inapoendelea kushinikiza mataifa mbalimbali kufanya vya kutosha kuhifadhi mazingira na kupunguza gesi yenye sumu kutoka viwandani.

Licha ya kuwa jamii isiyotambuliwa sana,  inakadiriwa kuwa  idadi yake ni kati ya watu 300-1,200 na inaendelea kuishi msituni.

Hata hivyo miaka ya hivi karibuni, maeneo yao yalichukuliwa na wafugaji na hivyo wamekuwa wakitatiza kuendelea na utamaduni wao.

Tuzo hiyo imepokelewa na kiongozi wa jamii hiyo  Ezekiel Phillipo, jijini New York nchini Marekani.

“Miaka kadhaa iliyopita, hatukuwa na wazo la kumiliki ardhi,” amesema Phillipo.

Hata hivyo, walipokea msaada kutoka kwa Shirika la Carbon Tanzania na kufanikiwa kumiliki Ekari 57,000 ya ardhi.

Kupitia ardhi hiyo, walianzisha mradi huo wa kutumia mabaki ya Carbon kutoka kwenye miti na misitu kujipatia riziki yao ya kila siku lakini pia kuhifadhi mazingira.

“Tulizindua mradi huu katika bonde la Yaeda mwaka 2013 na kumekuwa tukiuza mabaki ya Carbon kutoka miti na misitu ili kulinda eneo letu, sisi huhifadi mazingira kwa sababu ndio njia pekee inayotusaidia ,” ameeleza Phillipo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.